Cape Verde yafuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza

Dismas Otuke
1 Min Read

Visiwa vya Cape Verde ndio taifa la pili dogo zaidi kuwahi kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kufuatia ushindi wa 3-0, dhidi ya Eswatini, katika mchuano wa kundi D uliochezwa jana jioni mjiini Pria.

Nchini hiyo yenye idadi ya watu wasiozidi nusu milioni iliongoza kundi hilo kwa pointi 23, alama 4 zaidi ya Cameroon waliotoka sare tasa nyumbani dhidi ya Angola.

Timu hiyo almaarufu Blue Sharks ilishinda mechi saba kutoka sare mbili na kupoteza mara moja kati ya mechi 10 ilizocheza katika hatua ya makundi.

Cape Verde ni timu ya sita ya Afrika kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao baada ya Morocco, Tunisia, Algeria, Misri na Ghana.

Makala ya 23 ya mwaka ujao ya Kombe la Dunia yataandaliwa kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, katika miji 16 ya mataifa ya Marekani,Kanada na Mexico yakishirikisha mataifa 48 kwa mara ya kwanza.

Share This Article