CAF yazindua mpira utakaotumika fainali za AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la Kandanda Barani Afrika (CAF), likishirikiana na kampuni ya PUMA, limezindua mpira utakaotumika kwenye Makala ya mwaka huu ya kipute cha AFCON nchini Morocco.

Mpira huo ujulikanao kama ITRI, umechukua sanaa ya kale ya Morocco ijulikanayo kama zellij ikiwa na ihara ya kuliunganisha bara zima la Afrika.

Zelij pia inatoa heshima kwa msanii aliyejumuishwa kwenye bendera ya Morocco.

Morocco itaandaa fainali za 35 za AFCON kati ya tarehe 21 mwezi ujao na Januari 18 mwaka ujao zikishirikisha mataifa 24.

Mpira huo umetengenezwa kwa teknolojia ya Oribita 6.

Share This Article