Shiriksho la Soka Barani Afrika (CAF), limekanusha madai yaliyoibuliwa na wauzaji tiketi wa mechi kati ya Kenya na Zambia Jumapili hii, kuwania kombe la CHAN.
Kwenye kikao na Wanahabari Jumatatu jioni CAF, imeionya kampuni ya MOOKH dhidi ya kueneza habari za kupotosha kuhusiana na tiketi za mechi hiyo.
Hapo awali, kampuni ya MOOKH ilikuwa imetoa ripoti mapema Jumatatu kuwa CAF ilisitisha uuzaji wa tiketi kutokana na visa kadhaa vya utovu wa usalama, katika mchuano wa Jumapili iliyopita kati ya Kenya na Morocco.
Harambee Stars inatarajiwa kumenyana na timu ya Chipolopolo kutoka Zambia, katika mchuano wa mwisho wa kundi A Jumapili ijayo kuanzia saa mbili usiku, katika uwanja wa michezo wa Kasarani.