Bunge la Uganda laidhinisha shilingi bilioni 8 kujenga viwanja vya AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Bunge la Uganda limeidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 8.5 za Kenya sawia na shilingi bilioni 257 za Uganda kwa ujenzi na ukarabati wa viwanja vitakavyoandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Fedha hizo zitatumika kukamilisha ujenzi wa uwanja wa Hoima, ujenzi wa uwanja wa Akii Bua, na kukarabati viwanja vya kufanyia mazoezi kwa mashindano ya CHAN mwaka huu na AFCON mwaka 2027.

Pesa hizo zilitayarishwa na kutolewa ndani ya kipindi cha saa 48 pekee.

Uganda itaandaa fainali za CHAN kwa pamoja na Kenya na Tanzania kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu, kabla ya kuandaa tena kipute cha AFCON mwaka 2027 kwa ushirikiano na mataifa hayo mawili jirani.

Share This Article