Bunduki 22, risasi zaidi ya 100 zasalimishwa Kerio Valley

Martin Mwanje
1 Min Read

Polisi katika eneo la Tot, kaunti ya Elgeyo Marakwet wamepokea bunduki 22 aina AK-47 na risasi 108 zilizosalimishwa kwa hiari na wakazi wa eneo hilo jana Jumatatu.

Silaha hizo zilisalimishwa kwa timu ya usalama wa kaunti kupitia ushirikiano wa kamati za amani katika kata za Ketut, Mokoro, Murukutwo, Chesuman, Mon, Chemwonyo, Chechan, na Koibirir.

Kwenye taarifa, Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS, inasema silaha hizo zimehifadhiwa mahali salama katika kituo cha polisi cha Tot.

NPS imetaja hatua hiyo kuwa ishara chanya inayoashiria dhamira ya jamii kuishi kwa amani, usalama na kusalimisha silaha kwa hiari.

Aidha, imepongeza umma, wazee na kamati za amani kutokana na juhudi zao za kuhakikisha amani inadumu katika eneo hilo na kuzitaka kuendelea na moyo huohuo.

Share This Article