Mabingwa mara tano wa Dunia Brazil, walifuzu kwa fainali za 23 za mwaka ujao baada ya kuwapiga Paraguay goli moja kwa bila mapema leo.
Goli hilo na vijana wa Samba lilipachikwa kimiani na Vinicius Junior, mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kudumu hadi kipenga cha mwisho.
Brazil wanajiunga na mabingwa watetezi Argentina na Ecuador kutoka Amerika Kusini ,kujikatia tiketi kwa Kombe la Dunia mwaka ujao.