Halmashauri ya dawa na sumu PPB imekanusha madai ya kuzuia kuagizwa kwa bidhaa zaidi ya 21,000 za dawa humu nchini Kenya.
PPB imetaja madai hayo kuwa ya uongo na yanayolenga kuzua taharuki kwa umma.
Bodi hiyo imeongeza kuwa ni sharti iidhinishe dawa kabla ya kuingizwa nchini kila baada ya miaka mitano kwa mujibu wa sheria zilizoko.
Aidha, PPB imewataka wadau wote wanaogiza dawa humu nchini kupata vibali vipya vya kuendesha biashara yao kufikia Disemba 31 mwaka huu.