Askofu David Kodia wa kanisa amewakemea viongozi wafisadi serikalini ambao ameutaja kuwa kizingiti kikuu maendeleo ya taifa.
Akiongoza ibada ya aliyekuwa Waziri Mkuu marehemu Raila Odinga katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo, Askofu Profesa David Kodia wa kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Bondo amesema ipo haja ya serikali kupigana dhidi ya ufisadi kama njia ya kumuenzi Raila.
Amemtaja Raila kuwa mfano mwema wa kuigwa humu nchini.
Umati wa waombolezaji ulisimama kumsifia askofu kwa ujumbe mzuri na kisajiri kukemea maovu ya kijamii.