Bintiye hayati Magufuli, ajitosa kuwania Ubunge Tanzania

Jesca amechukuwa fomu za kuwania kiti hicho rasmi leo Jumamosi Juni 28.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jesca Magufuli bintinye  Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, amejitosa kuwania ubunge wa viti maalum kupitia umoja wa vijana wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CCM.

Jesca amechukuwa fomu za kuwania kiti hicho rasmi leo Jumamosi Juni 28.

Jesca ni Binti ambaye amejipambanua kama sauti ya matumaini kwa Vijana na Wanawake wa Tanzania akisimamia maadili, haki na maendeleo jumuishi ambapo amelenga kupeleka nguvu mpya ya kijana Bungeni, kusimamia ajenda za maendeleo kwa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla huku akihakikisha UVCCM inasikika, inaonekana na inawakilishwa kwa heshima katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nipo tayari kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu, umoja na kwa kutanguliza maslahi ya Vijana na Wanawake, Geita inapeleka sauti ya mabadiliko chanya,” amesema Jesca Magufuli mara baada ya kuchukua fomu hiyo leo.

Uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeratibiwa kuandaliwa Oktoba 28 mwaka huu.

Share This Article