Binti ya Paul Biya ashauri wananchi wasimpigie kura

Marion Bosire
1 Min Read
Rais Paul Biya wa Cameroon na binti yake Brenda

Binti ya Rais wa muda mrefu wa Cameroon Paul Biya aitwaye Brenda Biya wa umri wa miaka 27,  ameshauri raia wa nchi hiyo wasimpigie kura babake katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Brenda alifanya hivyo kupitia kwa video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ambapo alielezea wazi msimamo wake wa kupinga utawala wake.

Mrembo huyo ambaye ni mwanamuziki wa mtindo wa rap kwa jina ‘King Nasty’ alisema kwamba amechoshwa na hali ya mambo nchini humo akilaumu usimamizi wa babake.

“Cameroon inateseka, vijana hawana ajira, maisha ni magumu, watu wanaishi katika umasikini mkubwa. Na yote haya ni kwa sababu ya uongozi mbovu wa serikali ya sasa” alisema Brenda kwa hisia kali.

Aliendelea kwa kumlaumu baba yake, Rais Paul Biya kwa kushindwa kuwaletea raia maendeleo na fursa bora za maisha hata baafa ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 43, tangu mwaka 1982.

Brenda alitumia fursa hiyo pia kuwaomba msamaha raia wa Cameroon kwa niaba ya familia yake akisema, “Naomba radhi kwa yale ambayo babangu na utawala wake wamewasababishia. Ni muda wa mabadiliko.”

Rai Paul Biya ambaye sasa ana umri wa miaka 92, alitangaza mwezi Julai mwaka huu kwamba atagombea tena urais kwa muhula wa nane.

Share This Article