Biden amkaribisha Trump Ikulu

Marion Bosire
1 Min Read

Rais Joe Biden alikutana na Rais mteule Donald Trump katika Ikulu ya Marekani jana Jumatano, hatua ya kwanza ya mchakato wa kupokezana mamlaka.

Biden alihakikishia Trump kwamba serikali yake iko tayari kumsaidia kwa lolote analohitaji kama rais mteule wa taifa hilo.

Walizungumza mbele ya wanahabari ambapo walisalimiana huku Biden akisikika akimpongeza Trump kwa ushindi kwenye uchaguzi huku akimkaribisha ikulu kwa mara nyingine.

Trump alikuwa ameandamana na Elon Musk ambaye tayari amemteua kuwa Mkuu wa Ofisi mpya ya ufanisi wa Serikali yake inayotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Januari mwakani 2025.

Rais mteule Trump ametangaza baadhi ya Mawaziri wake anapoanza kuunda serikali yake.

Alikuwa hajatokea hadharani tangu alipohutubia wafuasi wake huko West Palm Beach baada ya kushinda uchaguzi.

Mkewe Melania Trump kwa upande mwingine anadaiwa kukataa mwaliko wa mke wa Biden Jill Biden mwaliko ambao ni tamaduni nchini Marekani.

Inaripotiwa pia kwamba Melania amesema kwamba hataishi katika Ikulu ya Whitehouse kikamilifu huku ikiaminika kwamba ataishi New York muda mwingine ambapo mwanawe Baron anahudhuria masomo ya chuo kikuu.

Share This Article