Bei ya umeme yatarajiwa kushuka hivi karibuni

Dismas Otuke
1 Min Read
Baadhi ya kaunti hapa nchini kukosa nguvu za umeme.

Bei ya kununua  nguvu za umeme inatarajiwa kushuka kwa kiwango kikubwa baada  ya Rais William Ruto, kusaini muswada wa ushuru wa umeme wa mwaka 2025 kuwa sheria.

Sheria hiyo inalenga kuondoa ushuru wa asilimia 25 kwa transformer za umeme na vipuri zinazoagizwa humu nchini.

Kulingana na taarifa ya Ikulu, kuondolewa kwa ushuru huo kutapunguza gharama ya mitambo ya transformer na vipuri vyake ambayo huongezwa kwa bei ya kununua umeme kwa sasa.

Serikali iliongeza bei ya transformer na vipuri vinvyoagizwa kutoka nje mwaka jana, ili kukuza na kuinua viwanda vinavyounda vifaa hivyo humu nchini.

TAGGED:
Share This Article