Bayern na PSG zanga’aa katika Kombe la klabu bingwa

Dismas Otuke
2 Min Read

Klabu za Bayern Munich ya Ujerumani na Paris saint Germain (Ufaransa), zimeanza vyema mawindo ya taji la klabu bingwa duniani nchini Marekani baada ya kulaza klabu za Auckland City (Marekani) na Atlético de Madrid mabao 10 na 4 kwa nunge mtawalia.

Ukurasa wa mabao ya Bayern ulifunguliwa na Kingsley Coman dakika za 6 na 21 kabla ya beki wa kulia Sacha Boey kuongeza la tatu dakika ya 18.

Michael Olise na Thomas Muller walifunga la nne na tano dakika za 20 na 45 mtawalia.

Zaidi ya hayo, Michael Olisea alirejea na kufunga kipindi hicho cha kwanza kwa kuongeza la sita dadika za 45+3.

Kwenye kipindi cha pili, maji yalizidi unga pale nguvu mpya Jamal Musiala alipotinga matatu dakika za 67, 73 ( tuta) na 84.

Mzee wa kazi Thomas Muller alifunga ukurasa huo daki za lala salama (89) kwa kufunga la kumi.

Katika Uga wa Rose Bowl, Fabián Ruiz na Vitinha wa Ureno waliwapa mabingwa wa Uropa mawili namo dakika za 19 na 45+1 mtawalia.

Kwenye dakika za 87 na 90+7, Senny Mayulu alitia la tatu naye Lee Kang-in akahitimisha kwa mkwaju wa adhabu.

Mechi nyingine ilichezwa usiku wa manane ambapo Batofogo ( Brazil) iliilaza Seattle Sounders FC (Marekani) mabao mawili kwa moja nazo Porto na Palmeiras zikatoka sare ya sufuri kwa sufuri.

Leo jumatatu, Chelsea itabisha dhidi wenyeji Los Angeles saa nne usiku, Boca junior na Benfica watafuata usiku wa manane kisha Flamengo wafunge dhidi ya El Tunis saa kumi alfajiri.

Share This Article