Barcelona watwaa La Liga kwa mara ya 28

Kwa jumla, Real Madrid wameshinda  la La Liga mara 36, wakifuatwa na Barcelona kwa mataji 28; nao Atletico Madrid wamevishwa ubingwa mara 11.

Dismas Otuke
1 Min Read

FC Barcelona ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uhispania-La Liga, kwa mara ya 28, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 jana usiku ugenini dhidi ya Espanyol, kiwarani RCD katika Derby ya Katalunya.

Barca wanaonolewa na Hansi Flick, waliingia katika mechi hiyo wakihitaji ushindi ili kuwazuia watani wao Real Madrid kuwa na fursa ya kutawazwa mabingwa.

Kipindi cha kwanza kiliishia sare tasa kabla ya wageni kuvunja safu imara ya Espanyol, kunako dakika ya 53, wakati Dani Olmo, alipompokeza pasi Lamine Yamal, akiyevurumiza tobwe hadi kimiani.

Fermin Lopez, alitanua uongozi wa Barca, katika dakka ya 5 ya nyongeza na kuwahakikishia ushindi pamoja na ubingwa wa ligi kuu msimu wa mwaka 2024/2025, kwa kuzoa jumla ya pointi 85 ,alama saba zaidi ya Madrid zikisalia mechi mbili kukamilika kwa  msimu.

Taji hiyo ilikuwa ya 28 kwa Barcelona na ya kwanza tangu msimu wa mwaka 2022/2023.

Kwa jumla, Real Madrid wameshinda  la La Liga mara 36, wakifuatwa na Barcelona kwa mataji 28; nao Atletico Madrid wamevishwa ubingwa mara 11.

Share This Article