Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hali nchini DRC

Tom Mathinji
2 Min Read
Wakazi wa Goma watoroka kufuatia mapigano kati ya vikosi vya DRC na waasi wa M23. Picha na Aljazeera.

Siku moja baada ya wapiganaji wa kundi la M23 kudai kuuteka mji wa Goma mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia Congo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kujadili mzozo huo kwa lengo la kudhibiti hali.

Wakazi wa Goma ambao ni mji mkuu mashariki mwa DRC walitoroka eneo hilo siku ya Jumatatu, baada ya kundi la M23 kudai wameuteka mji huo kutoka kwa majeshi ya DRC, huku mapigano yakiendela licha ya wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwataka waasi hao kuondoka.

Mkutano huo wa Baraza la Usalama la UN ambao uliitishwa na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, utaandaliwa leo Jumaane, kujadili mgogoro huo.

Hata hivyo, mkutano huo unajiri huku waziri wa mambo ya nje wa DRC Therese Kayikwamba Wagner, akisema hakufurahishwa na taarifa ya Baraza la Usalama la UN iliyotolewa Jumapili, ambayo ilitaka kujiondoa kwa “vikosi vya nchi za nje” kutoka nchi yake ambayo ni tajiri ya madini.

Serikali yangu inaeleza kufadhaishwa na jinsi Baraza la Usalama limetoa taarifa rahisi, isiyo wazi, na isiyo na maana,” alisema, na kuongeza kuwa Rwanda inahitajika kutambuliwa wazi kama “mshambuliaji.

Kupitia kwa ukurasa wa X, msemaji wa serikali Patrick Muyaya aliwahimiza wakazi wa Goma kusalia nyumbani, huku akiwataka raia wa Congo walioko nje ya nchi hiyo kutafuta uungwaji mkono wa nchi yao.

TAGGED:
Share This Article