Baraza la madhehebu Uganda,  lapiga marufuku siasa kanisani

Waliongeza kuwa wanasiasa wako huru kuhudhuria ibada na kuombewa, ila wasipige siasa wakiwa kwenye maabadi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Baraza la madhehebu nchini Uganda (IRCU), limepiga marufuku siasa ndani ya kanisa kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Katika uamuzi huo wa pamoja ulioafikiwa Mei 15, baraza hilo liliamuru kuwa hakutakuwa na fursa kwa wanasiasa kufanya kampeni kwenye maabadi, ikiwemo makanisa na misikitini.

Waliongeza kuwa wanasiasa wako huru kuhudhuria ibada na kuombewa, ila wasipige siasa wakiwa kwenye maabadi.

Uganda imeratibiwa kuandaa uchaguzi mkuu Januari 12 mwakani huku Rais wa sasa Yoweri Kaguta Museveni, aliye na umri wa miaka 80, na ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, atawania muhula mwingine wa miaka mitano.

TAGGED:
Share This Article