Barabara kadhaa kufungwa jijini kupisha Nairobi city Marathon

Waiyaki way – kutoka barabara ya Musa Gitau hadi mwingilio wa Expressway kuanzia saa sita usiku hadi saa nne mchana jumapili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Barabara kadha jijini Nairobi zimeratibiwa kufungwa kati ya saa nne usiku Jumamosi na saa tisa Jumapili kupisha makala ya nne ya mashindano ya mbio za masafa marefu za jiji la Nairobi.

Barabara hizo zinajumuisha;Expressway – kutoka James Gichuru hadi uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta kuanzia saa nne usiku jumamosi hadi jumapili saa tisa alasiri.

Waiyaki way – kutoka barabara ya Musa Gitau hadi mwingilio wa Expressway kuanzia saa sita usiku hadi saa nne mchana jumapili.

Kivukio cha barabara ya Mombasa na Southern Bypass Likoni – njia ya kutoka katika mzunguko wa eneo hilo na inayoingia jijini kuanzia saa sita usiku hadi saa tano mchana jumapili.

Uhuru Highway – baina ya Southern Bypass na mzunguko wa barabara ya Langata.

Vile vile itafungwa kati ya mzunguko wa Bunyala na Kenyatta Avenue.

Kenyatta Avenue – kati ya hoteli ya Pan Afric na Uhuru Highway kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi usubuhi jumapili.

Kufuatia hali hii, idara ya trafiki imewashauri watumizi wa barabara hizo kutumia njia mbadala.

Share This Article