Maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria kwenye barabara ya Kakamega-Mumias wamenasa bangi yenye uzito wa kilo 159.15.
Thamani yake inakadiriwa kuwa shilingi milioni 4.7.
Bangi hiyo ilipatikana ikiwa kwenye gari jeusi lililoachwa barabarani aina Toyota Fileder.
“Baada ya kulikagua, maafisa walitambua bangi ikiwa imewekwa kwenye magunia 7 na uzito wake ukiwa kilo 159.15. Ilikadiriwa kuwa yenye thamani ya shilingi milioni 4.7,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi kwenye taarifa.

Gari hilo lilivutwa hadi kituo cha polisi cha Kakamega huku uchunguzi wa kubaini mmiliki wake ukianzishwa.
