Bangi ya maelfu ya pesa yanaswa Kiambu

Martin Mwanje
1 Min Read

Polisi katika kaunti ya Kiambu wamefanikiwa kunasa bangi yenye thamani ya shilingi mia moja na nane elfu (108,000) katika kijiji cha Ruthiru, wadi ya Riabai.

Mshukiwa mkuu, Ann Njeri, mwenye umri wa miaka 20, alikamatwa akiwa katika harakati za kusambaza dawa hiyo haramu.

Mama yake pia anazuiliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kiambu, Francis Njomo, amesema operesheni dhidi ya mihadarati inaendelea, na ameonya kuwa yeyote atakayepatikana akijihusisha na ulanguzi au utumiaji wa dawa hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wameelezea hofu yao kuhusu kuongezeka kwa matumizi ya bangi miongoni mwa vijana, wakidai kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya upili ya Kinap hununua dawa hizo.

Polisi wamewataka wananchi kushirikiana nao kwa kuwafichua wahusika ili kusaidia kukomesha biashara hiyo haramu.

TAGGED:
Share This Article