Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino,amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha ugavana katika Gatuzi la Nairobi mwaka 2027.
Owino, hata hivyo, amesema kuwa yuko tayari kugombea kiti hicho kwa tiketi yoyote iwe ODM au bila.
Mbunge huyo anapania kumbwaga Gavana Jonson Sakaja wa cha UDA, katika kivumbi hicho cha mwaka 2027.
Owino amekuwa mhakiki wa uongozi wa chama cha ODM tangu mwaka jana, wakati chama chake kilipotangaza kushirikiana na serikali ya Kenya Kwanza.