AzureDé awasili Kenya kwa ziara

Marion Bosire
1 Min Read

Mwimbaji wa Afrika Kusini AzureDé yuko jijini Nairobi nchini Kenya alikowasili jana kwa ajili ya ziara yake.

AzureDé ambaye jina lake halisi ni Naledi Myongwane ni mwimbaji anayekua haraka katika tasnia ya muziki na alijipatia umaarufu ndani na nje ya Afrika Kusini kwa nyimbo zake kama, “Blow My Mind”, “Sondela” na “Helele”.

Alizaliwa na kulelewa katika mkoa wa KwaZulu-Natal, na kutokana na asili yake huwa anachanganya mitindo ya kiasili ya muziki na mitindo ya kisasa.

AzureDé ameibuka kupendwa sana na wapenda muziki kutokana na mtindo wake wa muziki na yuko nchini Kenya kwa ajili ya mahojiano kwenye vyombo vya habari kutangaza kazi zake.

Wimbo wake wa “Blow My Mind” ulienezwa sana kupitia mtandao wa kijamii wa TikTok ambapo ulisikilizwa zaidi ya mara laki moja katika muda wa wiki moja tu.

Share This Article