AY na Alpha wafiwa na babu yao

Marion Bosire
1 Min Read

Msanii maarufu wa muziki nchini Tanzania Allen Yessayah maarufu kama AY na mwenzake wa Rwanda Alpha Rwirangira wanaomboleza kifo cha babu yao mpendwa.

Jumanne Septemba 2, 2025, wawili hao walichapisha taarifa za kifo cha mzee huyo aliyekuwa na umri wa miaka 103, kwenye Instagram.

Alpha aliandika ujumbe wa kuwomboleza babu yake akimuaga kwa maneno, “Mpaka tutakapokutana tena kwenye maisha yajayo, Babu”.

AY naye alichapisha picha akiwa na mzee huyo na kuandika, “Pumzika kwa Amani Babu Yangu Kipenzi..Mwenyezi Mungu amekujalia miaka 103 ya kuishi..Ni baraka kubwa kwako na kwetu pia..nitakuomboleza hadi nitakapojiunga nawe”.

Mzee huyo ametajwa kuwa mtu aliheshimika kwa hekima yake, ujasiri, na mchango wake katika kulea vizazi vya mafanikio, ikiwa ni pamoja na kushuhudia wajukuu zake wakipaa kimataifa kupitia muziki na sanaa.

Share This Article