Awamu ya kwanza ya uuzaji tiketi za fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON imefunguliwa leo Jumatatu, siku 69 kabla ya kuanza kwa makala ya 35 ya kindumbwendumbwe hicho.
Mashabiki walio na kadi za Visa wamepewa saa 48 za kununua tiketi hizo kabla ya kufunguliwa kwa mashabiki wengine kuanzia Jumatano hii.
Ili kurahisisha ununuzi wa tiketi, mashabiki na kamati andalizi wamezindua APP inayojulikana kama YALLA App, ambayo pia itatumika kutuma maombi ya viza ya usafiri kuingia nchini Morocco.
Kipute cha AFCON kitaandaliwa Morocco kati ya Disemba 21 mwaka huu na Januari 18 mwaka ujao kikishirikisha mataifa 24.