Papa Leo wa 14 amebuni Dayosisi mpya Kapsabet na kufikisha 28 idadi ya dayosisi za Kanisa Katoliki zilizopo humu nchini.
Dayosisi mpya ya Kapsabet imebuniwa kutoka kwa Dayosisi Katoliki ya Eldoret na itahudumia kaunti yote ya Nandi.
Papa Leo amemteua John Kiplimo Lelei kuwa Askofu mwasisi wa dayosisi hiyo.
Lelei kwa sasa ni Askofu wa Eldoret.
Askofu Lelei mwenye umri wa miaka 66 alizaliwa Agosti 15, 1958 huko Soy, katika Dayosisi Katoliki ya Eldoret.
Alisomea Falsafa katika Seminari ya Mtakatifu Augustine huko Mabanga na teolojia katika Seminari ya Mtakatifu Thomas Aquinas jijini Nairobi.
Alitawazwa kuwa kasisi Oktoba 26, 1985 kuhudumu katika Dayosisi Katoliki ya Eldoret.