Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Joseph Kabila amewasili katika mji unaokaliwa na waasi wa Goma, siku chache baada ya Bunge la Senate kumvua kinga dhidi ya kushtakiwa.
>Kuwasili kwa Kabila Jijini Goma kulitangazwa na kundi la waasi la M23, hata ingawa halikukiri mara moja ikiwa yeye ni miongoni mwa viongozi wake.
Kabila amehusishwa na kundi hilo la M23, na hiyo ndiyo sababu ya kuondolewa kwa kinga yake dhidi ya kushtakiwa ili aweze kufunguliwa mashtaka ya kushiriki uhaini.
Kabila amerejea nchini DRC hizi majuzi kutoka uhamishoni Afrika Kusini, akisema anarejea ili asaidie kupatikana kwa amani nchini mwake.
Tangu kuwasili kwake nchini DRC, Kabila ameshtumu serikali kuu kwa kutenga eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.