Aliyekuwa Mkuu wa Polisi Nairobi, Anthony Kibuchi, afariki

Kibuchi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 67, alifahamika kwa kuwa mchapakazi bora na aliyekuwa na msimamo mkali dhidi ya uhalifu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa Mkuu wa Polisi eneo la Nairobi, Anthony Kibuchi, ameaga dunia katika hospitali ya rufaa na mafunzo ya chuo kikuu cha Kenyatta, alikokuwa anapokea matibabu.

Kibuchi aliripotiwa kuaga dunia Mei 13, kutokana na saratani ya tezi licha ya madaktari kutangaza kuwa alikuwa amepona saratani hiyo mwaka 2022.

Marehemu alistaafu kutoka kikosi cha polisi mwaka 2013, na kuhamia nyumbani kwake Kianugu, kaunti ya Kirinyaga.

Kibuchi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 67, alifahamika kwa kuwa mchapakazi bora na aliyekuwa na msimamo mkali dhidi ya uhalifu.

Mwendazake alihudumu katika nyadhfa kadhaa katika idara ya Kenya Police, ikiwemo Mkuu wa Polisi mikoani Nyanza na Kaskazini mashariki, kabla ya kuhamishiwa Nairobi alipokuwa PPO baina ya mwaka 2009 na 2013.

Share This Article