Aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo amefariki

Tom Mathinji
1 Min Read

Aliyekuwa mbunge wa Lugari Cyrus Jirongo ameaga dunia, baada ya kuhusiks kwenye ajali ya barabarani.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Karai, kaunti ndogo ya Naivasha kaunti ya Nakuru.

Akithibitisha ajali hiyo, Afisa Mkuu wa polisi wa trafiki eneo la Rift Valley Sarah Chumo, alisema ajali hiyo ilitokea Jumamosi saa tisa alfajiri kwenye barabara kuu ya Nairobi–Nakuru.

Kulingana na afisa huyo wa polisi, Jirongo alikuwa akielekea kutoka upande wa Nairobi kabla ya kugongana ana kwa ana na basi lililokuwa likielekea upande wa pili.

Jirongo alikuwa peke yake wakati wa ajali hiyo.

Jirongo alikuwa mbunge wa Lugari kati ya mwaka 1997 hadi  2002 na tena kati ya 2007 hadi  2013.

Share This Article