Ajuza aumiza wajukuu na kujitoa uhai Nyandarua

Marion Bosire
1 Min Read

Ajuza wa umri wa miaka 65 alishambulia wajukuu wake watatu kwa shoka kabla ya kujitoa uhai huko Kipipiri kaunti ya Nyandarua, kisa ambacho kimeacha wengi vinywa wazi.

kulingana na majirani, kisa hicho kilitokea asubuhi ya Novemba 10, 2025, ambapo ajuza huyo aliyekuwa na ghadhabu alijihami kwa shoka na rungu kabla ya kushambulia watoto hao.

Wajukuu hao wa umri wa miaka 18, miaka 9 na miaka minane wanaripotiwa kuachwa na majeraha mabaya.

Maafisa wa upelelezi wa jinai wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho huku kilichomchochea nyanya huyo aliyetambuliwa kama Esther wanjiku kikiwa bado hakijulikani.

Baada ya kutekeleza unyama huo, mama huyo anaaminika kuingia kwenye nyumba yake na kujitia kitanzi, polisi wakiripoti kupata mwili wake ukining’inia kutoka kwenye paa.

Watoto hao walipelekwa katika hospitali ya North Kinangop kwa matibabu ambapo wanaripotiwa kuwa imara na mwili wa nyanya yao ukapelekwa katika hifadhi ya maiti ya taasisi hiyo ya afya ukisubiri upasuaji.

Share This Article