Aibu! Umeme watoweka hospitalini Muhimbili kwa saa 15, wagongonjwa wataabika

Zaidi ya wagonjwa 200 waliokuwa wakipokea matibabu ya kuchuja damu walijipata mashakani wakati wa kupotea kwa umeme Jumapili saa tatu usiku, na hadi kufikia Jumatatu jioni haukuwa umerejeshwa katika maeneo yote.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wagonjwa wamehaha katika hospitali ya taifa ya Muhimbili nchini Tanzania, baada ya kutoweka kwa nguvu za umeme kwa saa 15.

Zaidi ya wagonjwa 200 waliokuwa wakipokea matibabu ya kuchuja damu walijipata mashakani wakati wa kupotea kwa umeme Jumapili saa tatu usiku, na hadi kufikia Jumatatu jioni haukuwa umerejeshwa katika maeneo yote.

Huduma zote katika hospitali hiyo zimekwama tangu kutoweka kwa umeme, huku baadhi ya wagonjwa wameelezea kupatwa na athari za kukosa huduma kama vile kuvimba miguu, wakiitaka serikali kutatua changamoto hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Hosptitali ya Muhimbili Aminiel Aligaesha, alikiri kutokea kwa hitilafu hiyo kabla ya maafisa kutoka kampuni ya umeme nchini humo Tanesco, kufika na kuerejesha umeme katika baadhi ya sehemu za Hospitali.

Share This Article