Afueni kwa wakulima baada ya korti kuruhusu usagaji miwa kwa muda

Martin Mwanje
1 Min Read

Wakulima wa miwa kutoka nyanda za chini za magharibi mwa Kenya wamepata afueni baada ya Mahakama Kuu ya Busia kusitisha agizo la Bodi ya Sukari nchini kutaka kufunga viwanda vya sukari katika maeneo hayo.

Wakizungumza nje ya Mahakama ya Busia, wakulima hao wakiongozwa na wakili Wangoi Kuria wameishtumu Bodi ya Sukari nchini kwa kutaka kuwadhululumu wakulima wa miwa nchini.

Aidha, wakulima hao wamepongeza uamuzi wa Jaji William Musyoka kwa kutupilia mbali kwa muda agizo la kufunga viwanda vya sukari kwa mda wa miezi mitatu huku wakishikilia kuwa madhumuni ya bodi hiyo ilikuwa na nia mbaya licha ya wao kutegemea kilimo hicho kwa mahitaji yao ya kila siku.

Wakati huo huo, wameitaka bodi hiyo kushirikiana na wakulima wanapotaka kutekeleza agizo kama hilo na kuongeza kuwa wangekadiria hasara ya miwa ambayo tiyari imekomaa.

Share This Article