Afrika Kusini watwaa Kombe la AFCON U20 kwa mara ya kwanza

Gomolemo Kekana alipachika bao pekee na la ushindi akifyatua tobwe kutoka nje ya kijisanduku kunako dakika ya 70 .

Dismas Otuke
1 Min Read

Afrika Kusini iliwashinda Morocco bao moja kwa bila na kutwaa kombe la Afrika kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, katika fainali iliyosakatwa jana usiku katika uwanja wa Juni 30 mjini Cairo Misri.

Kombe hili ni la kwanza kwa timu ya Afrika Kusini ya wanaume tangu Bafana Bafana watawazwe mabingwa nyumbani mwaka 1996.

Gomolemo Kekana alipachika bao pekee na la ushindi akifyatua tobwe kutoka nje ya kijisanduku kunako dakika ya 70 .

Mabingwa mara saba Nigeria walinyakua nishani ya shaba baada ya kuwalemea wenyeji Misri mabao 4-1, kupitia mikwaju ya penati baada ya sare ya bao 1-1.

Afrika Kusini, Morocco, Nigeria na Misri watawakilisha Afrika kwenye fainali za 24 za Kombe la Dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 baina ya Septemba 27 na Oktoba 19 mwaka huu nchini Chile.

Share This Article