Afrika Kusini na Ghana watinga nusu fainali WAFCON

Kipute hicho kitarejea Jumanne Julai 22, Nigeria wakipimana nguvu na Afrika Kusini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Afrika Kusini, Banyana Banyana na Ghana, walijikatia tiketi kwa nusu fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake Jumamosi usiku, baada ya kushinda kupitia changamoto ya penati.

Afrika Kusini waliishinda Senegal penati 4-1, katika robo fainali ya mwisho katika uwanja wa Honneur mjini Oudja, baada ya timu zote kutoka sare tasa.

Ghana pia walihitaji penati ili kuwashinda Algeria mabao 4-2,kufuatia sare tasa katika uwanja wa manispaa wa Berkane.

Kipute hicho kitarejea Jumanne Julai 22, Nigeria wakipimana nguvu na Afrika Kusini.

Fainali itapigwa Jumamosi ijayo Julai 26.

 

Share This Article