Algeria almaarufu Desert Foxes na Bafana Bafana kutoka Afrika Kusini wametoka sare ya bao moja, katika mchuano wa kundi C uliopigwa leo Ijumaa katika uwanja wa Nelson Mandela Namboole mjini Kampala Uganda.
Abdennour Belhocini aliwaweka Algeria mbele kunako dakika ya 29, kabla ya Thabiso Kutumela kusawazishia Afrika Kusini katika dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili timu zote zilicheza kwa tahadhari kubwa na mechi ilimalizikia sare.

Algeria waliomaliza wa pili katika makala ya mwaka 2022 wakiwa nyumbani, wanaongoza kundi C kwa pointi 4,wakifuatwa na Guinea kwa alama 3 huku Afrika Kusini ikiwa na alama moja.
Bafana Bafana watarejea uwanjani Agosti 11 dhidi ya Guinea katika mechi ya pili wakati Algeria wakipimana nguvu na Guinea tarehe 15.