Afisa mkuu wa ujasusi wa Ukraine, ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Kyiv, maafisa wamesema.
Afisa huyo wa Huduma ya Usalama ya Ndani ya Ukraine alipigwa risasi mara kadhaa kwenye eneo la kuegesha magari, baada ya mtu mmoja ambaye bado hajajulikana kumkaribia na kumpiga risasi, kisha akatoroka eneo la tukio.
Kanda za video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijami zinaonyesha jinsi tukio hilo lilivyotokea.
Shirika la kijasusi halikumtambua mwathiriwa, ingawa vyombo vya habari vya Ukraine vimemtaja kama Kanali Ivan Voronych.
Huduma ya Usalama ya Ndani ya Ukraine inahusika kikamilifu na usalama wa ndani na kupambana na ujasusi lakini tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi mnamo 2022, pia imehusika pakubwa na mauaji na mashambulizi ya hujuma ndani ya ndani ya Urusi.