Spika wa Bunge wa Taifa Moses Wetang’ula amewataka wanasiasa kukoma kuingilia kati utendakazi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), na badala yake kuiacha itekeleze majukumu yake kitatiba.
Alikuwa akihutubu katika hafla iliyoandaliwa katika eneo bunge la Kilgoris siku ya Jumapili alipohudhuria ibada katika kanisa la Ilchartuiyani Church of God.
Wetang’ula akitumia fursa hiyo kuwatahadharisha wanasiasa dhidi ya matamshi ya chuki.
“Ingawa tumechelewa kuratibu mipaka, nina imani IEBC bado ina uwezo wa kufanya hivyo kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027 ili kuhakikisha maeneo yote yanapata usawa wa uwakilishwaji.”
Hata hivyo, Wetang’ula ameondolea mbali uwezekano wa kubuniwa kwa maeneo bunge mapya kuongeza kwa 290 ya sasa, ila akasema wadi huenda zikaongezwa ili kuleta huduma karibu na wananchi.
Pia amewataka wabunge kupitisha mswada wa kuiongezea IEBC IEBC wakati utakapowasilishwa bungeni ili kurahisisha majukumu ya tume hiyo.