Gavana wa Kwale Fatuma Achani, amefungua rasmi wodi ya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Mwanda kilichoko Mwavumbo, eneobunge la Kinango.
Kituo hicho kinahudumia takriban wakazi 6,900 kutoka vijiji vinane vya eneo hilo, ambavyo ni Mwanda A, Mwanda B, Mwanda C, Dzombo A, Dzombo B, pamoja na Mwavumbo A na Mwavumbo B.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi, Gavana Achani alisisitiza kuwa serikali yake imejizatiti kuendelea kuboresha sekta ya afya ili kuhakikisha wakazi wa Kwale wanapata huduma bora za matibabu bila vikwazo.
Hadi kufikia sasa, serikali ya kaunti ya Kwale imejenga jumla ya vituo vya afya 178 na kuwaajiri wahudumu wa afya wapatao 1,800.
Wakazi wa eneo hilo wamepongeza juhudi za serikali ya kaunti ya Kwale katika kuboresha sekta ya afya na kuimarisha upatikanaji wa huduma za matibabu.