Achani aendelea kuboresha sekta ya afya Kwale

Martin Mwanje
1 Min Read
Gavana wa Kwale Fatuma Achani akizindua ujenzi wa jumba la kuhudumia wagonjwa katika hospitali ya Samburu

Gavana wa Kwale Fatuma Achani amezindua ujenzi wa jumba la kuhudumia wagonjwa katika hospitali ya Samburu ili kuhakikisha huduma bora za afya kwa wakazi wa kaunti ndogo ya Samburu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Achani amedokeza kuwa tayari eksirei imeletwa katika hospitali hiyo na punde ujenzi wa jumba hilo utakapokamilika, kutakuwa na maabara ya kisasa katika hatua itakayowapunguzia dhiki wakazi wa Samburu kusafiri mwendo mrefu kusaka huduma hizo.

Wakati uo huo, Gavana huyo amewataka wakaazi wa eneo hilo kujitokeza na kufanyiwa ukaguzi wa kiafya katika kambi ya matibabu ya bure inayoendelea katika hospitali hiyo inayodhaminiwa na serikali ya Kwale ikishirikiana na jeshi la majini la Kenya Navy.

Kufikia sasa, serikali ya Kwale imejenga na kuboresha vituo vya afya 178 kuajiri wahudumu wa afya zaidi ya 1,800 na pia maafisa wa afya wa nyanjani zaidi ya 1,600 ili wakazi wa Kwale wapate huduma bora za afya.

TAGGED:
Share This Article