Mtoto wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Ali Hassan Mwinyi, Abbas Mwinyi, kakaye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, amefariki dunia mapema Alhamisi Septemba 25.
Abbas Mwinyi alifariki katika hospitali ya Lumumba mjini Unguja.
Hadi kifo chake, Abbas Mwinyi, ambaye ni mtoto wa mstaafu marehemu Mzee Mwinyi, alikuwa msemaji wa familia mara baada ya kifo cha Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Abbas Ali Hassan Mwinyi alikuwa mwanasiasa na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM na alichaguliwa kuwa mbunge wa Fuoni kati ya mwaka 2015–2020.
Aidha, alikuwa msomi, rubani wa ndege na nahodha wa meli.