Washukiwa wawili wa mauaji wakamatwa kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wa mauaji wakamatwa Kirinyaga.

Maafisa wa polisi kaunti ya Kirinyaga, wamewakamata washukiwa wawili wanaodaiwa kumuua Margaret Wandauma Maina mwenye umri wa miaka 72.

Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana Disemba 14, 2025 kwenye kichaka katika kijiji cha Kegua, kaunti ndogo ya Kerugoya Mashariki, baada ya maafisa wa polisi kuarifiwa na wananchi.

Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, ilisema kuwa baada ya mwili huo kupatikana, maafisa walianzisha uchunguzi mara moja, na kufanikisha kukamatwa kwa James Njiru Murimi mwenye umri wa miaka 42 na mshirika wake  Peter Mbogo Wanjerima, mwenye umri wa miaka 35

Habari za awali zinaashiria kuwa marehemu alionekana mara ya mwisho katika kituo cha kibiashara cha Muthigiini Disemba 13, 2025.

Kulingana na maafisa wa polisi, mwili wa Wandauma ulikuwa na majeraha kwenye kichwa chake.

Washukiwa hao wanazuiliwa kwenye korokoro za polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani.

TAGGED:
Share This Article