Mvua kubwa imesababisha mafuriko katika eneo la Gaza, huku zaidi ya 800,000 wakitatozika.
Mvua kubwa na dhoruba kali katika eneo hilo, zimesababisha majengo kadhaa kuporomoka.
Maji yameendelea kutiririka kupitia nafasi zilizo wazi kwenye hema ambalo Ghadir al-Adham anaishi na mumewe na watoto sita katika Jiji la Gaza.
Familia yake imekimbia makazi yao baada ya vita, na inasubiri ujenzi upya uanze.
Miezi miwili baada ya usitishwaji mapigano uliosimamiwa na Marekani, Gaza imesalia katika awamu ya kwanza ya mpango wa amani wa Donald Trump,huku eneo lake likigawanywa kati ya pande zinazozozana, watu wake walihamishwa bado wamezungukwa na mabaki ya vifusi.