Sherehe ya Jamhuri yaandaliwa uwanjani Nyayo

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais William Ruto Leo Ijumaa atawaongoza Wakenya kuadhimisha sherehe za 62 za Jamhuri katika uwanja wa Taifa wa Nyayo.

Maudhui ya mwaka huu ni Utalii, Wanyamapori na Maendeleo.

Maelfu ya wananchi waliwasili mapema kwenye uwanja huo, tayari kwa sherehe hiyo.

Kamishna wa kaunti ya Nairobi Gilbert Kitiyo, amesema usalama umeimarishwa ndani na nje ya Nairobi, huku madereva wanaotumia barabara kuu ya Express Way na barabara ya Lang’ata wakishauriwa kutarajia msongamano

Sherehe za Jamhuri huandaliwa kila Disemba 12, kuadhimisha siku ambayo Kenya ilipata uhuru wake , mwaka mmoja baada ya kupata utawala wa ndani.

Share This Article