Mbunge mteule Denar Joseph Hamisi ameaga dunia, hayo yametangazwa na spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula.
“Ni kwa huzuni kubwa natangaza kifo cha mbunge mteule Denar Joseph Hamisi, ambaye ametuacha leo asubuhi,” alisema Wetang’ula kupitia ukurasa wa X Jumamosi asubuhi.
Wetang’ula aliongeza kuwa Hamisi alihudumia taifa hili kwa kujitolea na unyenyekevu mkubwa, hasaa akiwa mwanachama wa kamati ya Michezo na Utamaduni na kamati teule kuhusu Utangamano wa Kitaifa na Fursa sawa.
“Kwa niaba ya Bunge la Taifa, jamii yote ya bune na mimi binafsi, natuma rambirambi kwa familia, marafiki na kwa wale wote waliotangamana naye,” aliongeza Wetang’ula.
Spika Wetang’ula amemteua Naibu kiongozi wa wengi Owen Baya kushirikiana na familia ya marehemu Hamisi,ili kufanikisha shughuli za mazishi.