Mwanamuziki wa Uganda Cindy Sanyu amezungumzia sababu za kutohusika kwake kwenye mikutano ya kampeni kama wasanii wengine nchini humo.
Alikuwa akizungumza kwenye mahojiano ambapo alisema kwamba hana nia ya kutumbuiza kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2026, hata ingawa kazi hizo zinalipa vizuri.
Cindy alisema kwamba ana mashabiki katika kila upande wa kisiasa nchini Uganda ambao wanajumuisha wanaounga mkono serikali, wanaounga mkono upinzani na wale ambao hawaungi mkono upande wowote.
Anaonelea kwamba kupanda kwenye majukwaa ya siasa huenda kukakwaza baadhi ya mashabiki wake ambao wamekuwa naye kwenye safari yake ya miongo miwili katika tasnia ya muziki.
Nembo yake anasema imegharimu muda na uwekezaji wa kiwango kikubwa na inafuata uthabiti, talanta na kujitolea.
Msanii huyo ambaye pia anahudumu kama rais wa chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA, aliangazia pia jinsi siasa huathiri fikra za mtu akisema mitazamo hubadilika kulingana na msimamo.
Alipoulizwa iwapo angependa kushiriki pambano la pili la muziki na hasimu wake Sheebah Karungi, Cindy alisema haitakuwa vyema kuaibisha mwanamke mwenzake mara ya pili.
Sheebah na Cindy waliwahi kuandaa pambano la muziki Septemba 15, 2023 katika uwanja wa Kololo