Rais Ruto awapokea Mabalozi wapya katika Ikulu ya Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto awapokea Mabalozi wapya sita.

Rais William Ruto siku ya Jumatatu alipokea vyeti vya utambulisho vya Mabalozi na Makamishna sita wakuu wapya katika Ikulu ya Nairobi, katika hafla inayonuiwa kuimarisha uhusiano wa kimataifa.

Mabalozi hao ni Adarsh Swaika (India), Vincenzo Del Monaco (Italy), Verónica García Gutiérrez (Costa Rica), Paul Evans Aidoo (Ghana), Gia Matcharadze (Georgia), na Lilly Stella Ngyema Ndong (Gabon).

Rais alisema Kenya inajizatiti kuimarisha uhusiano wa kimataifa kote duniani, akisisitiza kwamba ushirikiano huo ni muhimu katika kuimarisha biashara, kuvutia uwekezaji  na kuimarisha maendeleo endelevu.

Alisema kuimarisha ushirikiano wa kimataifa,  kutafanikisha ukuaji wa kiuchumi wa taifa hili  na kufanya Kenya  kuwa mshirika muhimu kwenye maswala ya kimataifa.

Rais  Ruto alisema ushirikiano huo ni jitihada za kuhakikisha  kuna manufaa kwa taifa hili kutokana na kuimarishwa kwa uchumi kupitia ushirikiano kwenye maswala kama vile teknolojia, miundo-mbinu  na uongozi.

TAGGED:
Share This Article