Wakazi wa shirikisho wataka eneo lao la kiutawala

Marion Bosire
1 Min Read

Wakazi wa eneo la Shirikisho na vijiji vilivyo karibu, katika eneo bunge la Garsen, Kaunti ya Tana River, waliandamana wakidai eneo lao litangazwe kuwa eneo rasmi la utawala.

Watu hao walisema wanataka wapatiwe lokesheni yao wakisema kwamba chifu wa eneo hilo amekuwa kikwazo kikuu na amekuwa akiwanyanyasa watu wa jamii hiyo.

Wakazi hao wanamshutumu chifu kwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi wakati wa usajili wa wanufaika waliokusudiwa kupokea mipango mbalimbali ya msaada wa kijamii.

Wanasema kuwa hatua hizo zimesababisha ukosefu wa haki, ubaguzi na kutokuwepo kwa usawa katika ugawaji wa huduma hizo.

Zaidi ya hayo, wameitaka Serikali ya Kitaifa kuingilia kati na kuhakikisha kwamba eneo lao linapewa hadhi rasmi ya eneo la utawala ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za serikali na kuimarisha usimamizi wa kiutawala katika ngazi ya mashinani.

Share This Article