Klabu ya mchezo wa raga ya Kabras ya wachezaji 15 kila upande kutoka Kakamega, imezidi kuonyesha tamaa ya kunyakuwa taji kuu la mchezo huo nchini (Kenya Cup) kwa mara nne mtawalia baada ya kuvuna ushindi wa pili wa mechi ya pili msimu huu ilipokichakaza chuo kikuu cha Daystar (Daystar Falcons) alama 50 kwa nunge mjini Athi River.
Kwenye ngarambe ya kwanza nyumbani dhidi ya majirani wao MMUST (Masinde Muliro University), Kabras ilipata ushindi mnene wa alama 67 kwa sita.
Katika nyuga zingine, Strathmore Leos iliiadhibu Nondies alama 32 kwa 30 wakati KCB ikiitafuna Kisumu RFC alama 41 kwa 10 nayo Blak Blad ikapata alama 21 dhidi ya 10 za Nakuru RFC.
Zingine zilizonga’aa wikiendi ni Menengai Oilers na Kenya Harlequins kwa alama 97 na 24 dhidi ya Impala RFC na MMUST waliopata alama sita na 13 mtawalia.