Bunduki 4, risasi 13 zasalimishwa North Rift

Tom Mathinji
1 Min Read
Bunduki 4, risasi 13 zasalimishwa North Rift. Picha/Maktaba.

Bunduki nne na risasi 13 zimesalimishwa katika kituo cha polisi cha Tangulbei kaunti ndogo ya Tiaty, katika kaunti ya Baringo.

Zoezi hilo linaonekana kuwa hatua kuu katika kurejesha utulivu eneo hilo la North Rift.

Asasi za usalama eneo hilo zinaongoza kampeni ya kusalimisha silaha, ambayo imenzaa matunda. Kwa sasa zaidi ya silaha 541 zimesalimishwa katika kaunti ya Baringo.

Maafisa wa usalama wamepongeza hatua hiyo, wakibainisha kuwa, kusalimisha silaha kwa hiari inaonyesha imani inayoongezeka kati ya jamii na asasi za usalama.

Maafisa wa usalama wamefanikiwa kupata risasi 1,739 na silaha tano, hii ikiashiria hatua katika kampeni ya kukabiliana na silaha haramu.

Maafisa wa usalama eneo hilo wamekuwa wakitoa wito kwa wakazi kuunga mkono, juhudi za zoezi hilo, wakitaja mpango huo kuwa muhimu katika kukabiliana nautovu wa usalama unaohusishwa na wizi wa mifugo na mizoz ya kijamii.

Share This Article