Mpiga ngoma Jellybean Johnson ambaye wengi wanafahamu kwa kuwa kwenye bendi ya ‘The Time’ ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 69.
Jellybean ambaye jina lake halisi ni Garry George Johnson alifariki ghafla Ijumaa usiku, kulingana na familia yake ambayo pia ilisema kwamba kilichosababisha kifo chake hakijabainika.
Mbali na kuwa mpiga ngoma wa pekee katika ‘The Time’, ambayo baadaye ilibadilisha jina kuwa ‘Morris Day and the Time na The Original 7ven’ marehemu msanii huyo alijulikana kama mvumbuzi muhimu wa kile kilichokuja kujulikana kama mdundo wa Minneapolis ambao ni mchanganyiko wa mitindo ya funk, rock na soul ya miaka ya 1970 na 1980.
Jellybean pia alikuwa mwanachama wa kundi lililoanzishwa na Prince liitwalo ‘The Family’ na mwimbaji Susannah Melvoin ametoa heshima kwa “ndugu” yake kwenye Instagram baada ya kifo chake cha ghafla.
Alimkumbuka kama mpiga gitaa mahiri, akisema… “oksijeni kwake ilikuwa pumzi ya ndani na nje ya kupiga gitaa.”
Aidha, alicheza kama toleo lake la kubuniwa katika filamu ya 1984 Purple Rain na alisaidia kutayarisha kibao cha Janet Jackson cha mwaka 1990 kilichoongoza orodha ya nyimbo bora cha ‘Black Cat’.
Familia yake imeiambia wanahabari kwamba Jellybean alipenda familia yake, marafiki zake na jiji la Minneapolis. Yeye ni mwanzilishi, pamoja na mpenzi wake wa zaidi ya miaka 20, Marty Bragg, na binti yake, wa Minneapolis Sound Museum.
Taasisi hiyo iliundwa kuhifadhi historia na urithi wa midundo ya Minneapolis. Jellybean alikuwa amesherehekea siku yake ya kuzaliwa alipofikisha umri wa miaka 69 wiki hii.