Mugaa: Bwawa la Thiba limeimarisha kilimo cha mpunga Mwea

Tom Mathinji
1 Min Read
Bwawa la Thiba limeimarisha kilimo cha mpunga Mwea.

Uzinduzi wa bwawa la Thiba limeimarisha kilimo cha mpunga katika neo la Mwea kaunti ya Kirinyaga, kulingana na waziri wa Maji na unyunyiziaji mashamba Maji mhandsi Erick Mugaa.

Akizungumza alipofanya ziara kwenye mpango wa unyunyizaji mashamba maji wa Mwea, waziri huyo alidokeza kuwa bwawa la Thiba sasa linawafaidi wakulima 15,905 katika ekari 31,000 zinaznonyunyizwa maji kwenye mpango huo.

“Hatua hii imefanikisha uzalishaji metrik tani 170,000 na kuwezesha mapato ya shilingi bilioni 25, huku shilingi bilioni 12.7 zikiwafikia wakulima moja kwa moja,” alisema waziri Mugaa.

Aidha, waziri huyo alisema ujenzi wa mfereji katika wadi ya Mutithi, utasaidia pakubwa katika uzalishaji wa zao hilo katika ardhi ya ekari  4,000.

Kulingana na Mugaa, mafanikio hayo yanaambatana na mpango mpana wa Rais William Ruto wa kupanua kilimo kupitia unyunyizaji maji mashamba, ili kuhakikisha utoshelevu wa chakula, kubuni nafasi za ajira na kuongeza mapato ya wakulima.

Share This Article