IEBC yakamilisha mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupiga kura

Tom Mathinji
1 Min Read
IEBC yakamilisha mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi kabla ya Chaguzi ndogo wiki ijayo.

Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka IEBC, imekamilisha utoaji mafunzo kwa maafisa wa usimamizi wa uchaguzi na manaibu wao, kabla ya kuandaliwa kwa chaguzi ndogo Novemba 27,2025.

Aidha, maafisa hao walikula kiapo, kuelezea kujitolea kwao kudumisha maadili, usawa na utaalam wakati wa mchakato wote wa uchaguzi.

“Hii inaongeza nguvu ahadi yetu ya kutekeleza uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika,” ilisema IEBC kwenye ukurasa wake wa X.

Tume hiyo iliongeza kuwa, huku ikiingia katika hatua zake za mwisho kabla ya chaguzi hixo ndogo, maafisa wake wako tayari kusimamia vituo hivyo vyote ambapo chaguzi hizo zitaandaliwa.

“Tume hii imejitolea kuhakikisha kila mpiga kura aliyesajiliwa anatekeleza haki yake,” iliongeza IEBC.

TAGGED:
Share This Article